shirika la Craft Silicon Foundation, linalomilikiwa na kampuni ya kuuza programu za kompyuta, limeanzisha mradi unaowawezesha vijana kujifunza kutumia komputa ndani ya basi ambalo ni darasa.
Basi hilo huhudumia vijana maskini katika mitaa ya Kawangware, Mukuru, Korogocho, Kibera na Mathare.
Priya Budhabhatti ambaye ni muanzilishi wa mradi huu amesema kuwa ameamua kuanzisha mradi huo kwa kuwa alikua akipata shida ya usafiri pindi anasoma, hivyo kuamua kuja na aidia hiyo.
Wanaotaka kunufaika huwasilisha maombi kwa wakfu huo na wakikubalika, huhudhuria masomo saa mbili kila siku.wenye basi, huwa kuna walimu wawili ambao huwapa mafunzo mafunzo ya msingi kuhusu kompyuta na jinsi ya kutumia programi tekelezi kama vile Microsoft Word, Microsoft Excel na Microsoft Access. na masomo hayo hutolewa bila malipo yoyote.
No comments