Posted by:
Unknown
Posted date:
12:21:00
/
Maelfu ya wa Marekani wameendelea kuandamana mjini New York kupinga amri ya Rais Donald Trump kuzuia mataifa ya Kiislam na Wakimbizi kuingia nchini humo kwa lengo la kuzuia ugaidi. Mataifa yaliyo zuiliwa ni
nchi za Iran, Iraq, Somalia, Sudan, Libya na Yemen.
waandamanaji wameandamana katka miji tofauti tofauti huku wengine wakielekea ikulu wakiwa na baadhi ya mabango yakisoma kuwa “No wall, no ban”, “No hate, no fear. Refugees are welcome here”,
KATIKA HATUA NYINGINE TAKRIBANI WATU MILIONI MOJA WAMETIA SAHIHI YA KUMZUIA TRUMP KUZURU UINGEREZA.
Zaidi ya watu milioni moja wa Uingereza wamesaini barua ya kutoa shinikizo kwa serikali ya Uingereza kusitisha ziara rasmi iliopangwa baadaye mwaka huu ya rais Donald Trump.
Barua hiyo iliyoandikwa kufuatia agizo la rais Trump dhidi ya wahamiaji, inaeleza kuwa kuja kwake kutamuaibisha Malkia Elizabeth.
Idadi ya watu wanaoendelea kusaini kupinga Mwaliko wa Trump nchini Uingereza inaendelea kuongezeka, tangu Marekani kuweka vikwazo dhidi ya wageni hatua iliyozua ghadhabu kote duniani.
Amri ya Trump: Ni nani anaathirika?
No comments