Followers

Theme images by tomograf. Powered by Blogger.

ENTERTAINMENT

GOSSIP

INTERNATIONAL NEWS

LOCAL NEWS

» » HIVI NI BAADHI YA VITU VIMPAVYO SIFA RAIS BARACK OBAMA KAMA KIONGOZI.




Rais Barack Obama ni Rais wa kwanza wa Marekani mwenye asili ya kiafrika yani African American kutawala taifa hilo. lifestyle ya maisha yake ndiyo inayompa sifa kama kiongozi rais huyo.  Rais Obama ni mwanasheria kitaaluma na alikuwa Muhadhiri akifundisha somo la sheria ya katiba katika chuo kikuu cha Chicago shule ya sheria kuwanzia 1992 - 2008. 

Hivi ni baadhi ya vitu ambavyo huvifanya na humfanya kupata sifa. 

Uongeaji wake;- kama mwanasiasa Obama hutoa sauti nzito na isiyetetemeka yani Loud and clear. katika mikutano yake na hata katika mazungumzo mbali mbali anayoyafanya kama Rais. hii huashilia usialiasi katika maamuzi yake na pia huashilia utekelezekaji wa vitu anavyo visema ama kuahidi.

Obama kupitia video mbali mbali ama kwa wale waliwezo kumuona live basi lazima utakili kua ni mtu wa ucheshi na utani mwingi sio tu kwa familia yake bali hata viongozi wanaomfata kidaraja na dunia kwa ujumla.

ni Rais anayependa micheza na burudani kwa ujumla kuna baadhi ya videos tumemshuhudia akicheza muziki, mpira wa kikapu na hata mpira wa miguu kama tulivyomshudia akimpa pasi Rais wetu mstaafu Muheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete pale Ubungo.



Ni mtu wa kuthubutu na nivigumu sana kwake kukata tamaa, kwa wasio fahamu Rais Barack alishawahi kugombea uongozi mwaka 2000 nchini marekani na akashindwa lakini hakukata tamaa aligombea awamu nyingine na kushinda.

Ni kiongozi mpenda demokrasia na hupenda sana kuona haki ikitendeka Rais Obama kupitia hotuba zake amekua mstari wa mbele kuhimiza viongozi wa Africa kufata misingi ya demokrasia  Chaguzi nyingi za marais wa Africa na ngazi zingine zimekuwa zikigubikwa na tuhuma mbali mbali kuhusu michakato ya uchaguzi.

Unaweza ukamuita masta wa kuongea kwa vitendo:- Ni Rais anayependa kutumia body language  katika hotuba zake hii inasaidia kuonesha kuwa anajua anacho kizungumza na hii staili hata wanafunzi wa vyuoni huwapa sifa mbele ya Wahadhiri wao pindi wakiwasilisha kazi zao kwa kuonge katika majukwaa ya madarasa yao.


Ni Rais anayependa watoto. ni nadra sana kumkuta Rais huyu akiwapita watoto bila kuwatania au kuwachekesha. wakati baadhi ya viongozi huwasalimia watoto pindi za uchaguzi. kitu ambacho huwafanya wapiga kura wao waamini wanafanya hivyo kwa nia ya kupata nafasi wanazo wania. Rais pia hujibu barua za watoto wanazo muandikia baadhi ya watoto hao ni Miss Flint Mari msichana wa miaka 8 huko marekani na Christopher Kule mvulana aliyejibiwa barua na Rais akiwa na miaka 10 kutoka nchini Uganda Kasese.


Staili yake ya kuvaa na kukunja shati la mikono mirefu nayo imempa sifa sana duniani ambapo watu wengi hutafsiri utayari wa kiongozi huyo kufanya kazi na kutumikia watu. picha nyingi zinamuonesha kiongozi huyo akikunja shati la mikono mirefu.
 

Vipo vitu vingi ambavyo Hot Bongo 255 ikiamua kuchambua basi ni vitabu kwa vitabu. Japo hatukatai kuwa Rais Obama kama binadam anamapungufu yake ila anastahili pongezi na watu wajifunze kutoka kwake kwa mazuri yake.

Mwaka huu mwezi wa kumi na moja Taifa hilo litafanya uchaguzi wa Rais mpya kati ya Hillary Clinton na Trump. Huku Barack Obama akimaliza muda wake.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

About the Author Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

No comments

Leave a Reply

MOVIE

VIDEO

FASHION

Cat-5

MUSIC