Followers

21 Mar 2017

BRAND NEW MUSIC VIDEO KUTOKA KWA NILLAN - NJENJE.

Msanii mpya wa Bongo fleva NILLAN ameachia ng...

21 Mar 2017

BRAND NEW MUSIC VIDEO KUTOKA KWA NILLAN - NJENJE.

Msanii mpya wa Bongo fleva NILLAN ameachia ng...

Theme images by tomograf. Powered by Blogger.

ENTERTAINMENT

GOSSIP

INTERNATIONAL NEWS

LOCAL NEWS

» » » KUTANA NA STORY YA UGUMU WA MAISHA YA MR IBU MUIGIZAJI KUTOKA NIGERIA ILIYOMSABABISHA KUTAKA KUJIUA.


Jina lake kamili ni John Okafor ila wengi hupenda muita MR. Ibu kutokana na movie iliyompa umaarufu aliyoigiza na Ukwa.

Kupitia kipindi cha Saturday Beats muigizaji huyo wa vichekesho ameeleza jinsi alivyo taabika mwaka 1997 mpaka kufikia hatua ya kutaka kujiua.

HOT BONGO inakupa full story ya maisha ya msanii huyo kama ifuatavyo.

“unajua nilipanga kujiua huko AJAO. Siku hiyo nilipanga kujiua kutokana na mazingira magumu yaliyo nikabili.

Siku tatu kabla nilikua sijala chakula na nilikua sina matumaini ya kupata chakula wiki moja mbele. Nilikuwa nikinywa maji tu na sikuwa napenda kubugudhi mtu.

Marafiki zangu wakaribu hawakujali usalama wangu japo kuwa walijua sikua vizuri kifedha. Nakumbukua tarehe 18 Desemba 1997 rafiki yangu niliyekuwa nikiishi kwake aliniambia asubuhi kuwa angesafiri kwao kwa ajiri ya chrismas na hakupenda mtu yeyote aingie chumbani kwake.

Nikamuhakikishia kuwa hakuna mtu atakayeingia chumbani kwake, lakini akasema kuwa hata mimi nitoke . nilimuambia kuwa sina sehemu yoyote ya kuishi na nilimsihi aendelee kuniamini kama kawaida na ningeendelea kumtunzia chumba chake. Japo nilikuwa mkubwa kwake, lakini nilifanya kazi zote za kufua kuosha vyomba nilifua mpaka nguo zake za ndani.

Nilifanya yote hayo ili niweze kupata pakulala, ila kwa hasira rafiki yangu alitoa vitu vyangu nje na kuvitupa na kuniambia niondoke kwake. Hivyo alifunga mlango wake na kuondoka.

Pale nilipokuwa nimekaa kwa mbele kulikuwa na kisima nilifikiria kuwa sio jambo jema kujirusha katika kisima na kuyamaliza maisha yangu kwa kujiua na endapo rafiki yangu angerejea nakukuta nimejiua angejisikia vibaya kwa kuamini kuwa yeye ndiye chanzo cha mimi kufanya hivyo. Hata watu walio kuwa wakitumia maji yale wangekuta maiti yangu wasingetumia maji yale.

Lakini nilikwenda kisimani na kufungua mfuniko wa kisima na pindi nikijiandaa kuruka nilipitiwa na picha ya mama katika fikra zangu. Nilirudisha mfuniko na kuwaza mama amejuaje kuwa nataka kujiua.
Mama yangu alikuwa hai kipindi hicho akiwa na miaka kama 80 hivi. Nilikwenda karibu na ukuta wa jirani na kuegemea Francis alikuwa akipiga nyimbo ya Michael Bolton “when am back on my feet again” nikachukua uamuzi wakuto jiua tena.

Baada ya hapo niliamua kuwa na lala chini ya uvungu wa lorry bovu sehemu ambayo mbwa walikuwa wakilala nilibaini kuwa ni mbwa walikuwa wakilala pale wakati wa kupasafisha. Ila sikua na namna zaidi ya kulala pale pale.

Usiku mmoja takribani mbwa 30 walikuwa wakibweka hivyo hakuna aliye lala nanilizamika kuhamisha makazi yangu, wakati nikihama nikaona kikundi cha watu wamekusanyika na nilipo sogea nikagundua kuwa ni maigizo na ndipo hapo nilipo muona Sandra Ezeh.

Sandra alipo niona alinikumbatia na kudai kuwa alikuwa shabiki mzuri wa maigizo yangu, hasa uhalisia wangu katika igizo la Ikuku (muda huu MR IBU aliigiza  lakini malipo hayakuweza mnufaisha). Aliniuliza kuwa kama nilikuwa nafanya chochote na nilopo mwambia kuwa nilikuwa sina kitu chochote alinisihi tukamuone boyfriend wake.

Nilikubali kwa vile kwa wakati huo nilikuwa na njaa kali sana. Hivyo tulienda na tulipofika kwake tukaambiwa amesafiri. Akaniomba twende kwa rafiki yake mwingine.

Tulikutana na mwanamke mmiliki wa bar niliomba chakula nikapewa nikala na kulala usingizi mzito sana. Nilipo amka nikaona kibao adetola street nikakumbuka kuna rafiki aliniomba nikaishi kwake nyumba namba 125. Nilikwenda na nikakuta rafiki yangu Frank amerejea kutoka London.

Frank alinitaka nikachukue mizigo yangu ili niishi nae. Nilifata mizigo na kurudi kwake na hapo ndipo alipo nikabidhi chumba katika ghrofa yake. Nilipiga magoti nakushukuru Mungu”.


Hii ndiyo story ya kusikitisha aliyopitia Muigizaji huyo kutoka Nigeria ambaye kwa sasa anamafanikio makubwa aliyo yapata kutokana na maigizo yake huku akifanya show nyingi ndani na nje ya Afrika. Hivyo hupaswi kukata tama katika maisha pambana kwa kila namna kuhakikisha unafanikiwa na unatimiza azma yako.
«
Next
TAZAMA NGOMA KALI ALIYO SHILIKISHWA VANESSA MDEE NA ICE PRINCE - NO MIND DEM.
»
Previous
TAZAMA VICHWA VYA HABARI VYA MAGAZETI YA LEO TAREHE 29/02/2017

About the Author Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

No comments

Leave a Reply

MOVIE

Cat-5

MUSIC