STENDI KUU YA MABASI DAR ES SALAAM KUJENGWA KATIKA KIWANGO CHA KIMATAIFA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam amefanya ziara ya kushtukiza tarehe 10 August 2016 katika Stendi ya Mabasi ya Mikoani (Ubungo terminal) ambayo inatarajiwa kuhamishwa kutoka Ubongo kwenda Mbezi mwisho. Mkuu wa mkoa katika ziara hiyo alizungumza yafuatayo:-
‘Shahuku yangu ni kuwa na stendi tofauti na tuliyonayo, nataka Dar es salaam iwe na stendi ya kimataifa na tayari tunalo eneo kule mbezi ambapo halmashauri ya jiji tayari ipo kwenye mchakato wa kukamilisha ujenzi huo‘
Nataka kuihamisha hii stendi ya ubungo ili tuepukane na kero ya kukutana na mabasi ya mwendo kasi kwakuwa nayo ni moja ya changamoto, duniani kote maroli yakiingia katikati ya mji hutumika kubeba mikate ajabu Dar es salaam maroli yanabeba ngano na makontena‘
‘Lakini kabla ya wiki hii haijaisha nataka kuona taa zote za ubungo zinawaka, sitaki kuviona vifusi katika eneo hili la stendi na baada ya siku 20 nitarejea kujionea utekelezaji wake kama umekamilika‘
‘Kuanzia leo ni marufuku mtu kupiga faini katika parking ya ubungo, lazima tuweke alama za eneo gani la kupaki na wapi sio eneo la kupaki na hili itaanza baada ya kukamilika kwa ugawaji wa maeneo hayo‘
No comments