LeoTarehe 2/Februari/2016 Muheshimiwa Mkuu wa Mkoa ametoa taarifa kuhusu utafiti wake wa mtandao wa wauza madawa ya kulevya.Paul Makonda ameamua kuchukua hatua ya kupambana na wafanyabiashara wa madawa hayo baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya hasa kwa vijana ambao ndio nguvu ya taifa.
- Kuna maeneo watu wanatuambia madawa ya kulevya wanayapata sehemu hizo, wamiliki wake kesho niwakute polisi, wasipokuja nitawafuata
- Kama unajua una eneo unafanya biashara za dawa za kulevya DSM natoa siku 7 biashara hii iishe, operesheni hii naiongoza mwenyewe
- Kama Kamishna Sirro na timu yake watashindwa kutokomeza dawa za kulevya DSM maana yake wamekosa sifa za kuendelea kuwa askari
- Watano tayari nimeshawakamata na wengine nimewakamata wakiwa na dawa za kulevya
1- Detective Koplo Noel (Kituo chake cha kazi ni Central Police Dar)
2- Dotto (Yuko Kituo cha Kijitonyama)
3- Mwingine anafahamika kama 'Makomeo' (Kituo cha Oyster-bay)
4- Glory (Yuko Kituo cha Kawe)
5- Inspector Fadhili (Yuko Kituo cha Kinondoni)
6- Steve (Kinondoni)
7- James (Kinondoni)
8- Ditective Koplo (Wille)
No comments