Posted by:
Unknown
Posted date:
22:37:00
/
Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un
amesema kuwa taifa lake linakaribia awamu ya kutengeza kombora la
masafara marefu ambalo lina uwezo wa kubeba bomu la nuklia.
Katika
hotuba ya kuukaribisha mwaka mpya iliopeperushwa hewani katika runinga
ya taifa
Bw Kim amesema kuwa Korea Kaskazini imeimarika kama taifa
lenye uwezo wa kinyuklia mwaka 2016.
Pyongyang imefanya majaribio
mawili ya kombora la kinyuklia katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita
ikiwa ni mojawapo ya majaribio yake makubwa kufikia sasa.
Hatua hiyo ilizua shutuma mbalimbali na kuvutia vikwazo vya kimataifa .
Haijulikani taifa hilo imekaribia kivipi kutengeza kombora la Kinyuklia ambalo linaweza kurushwa na kufika Marekani.
No comments