Matokeo yaliyokuwa yakisubiriwa kwa hamu hatimaye yatoka huku mfanyabiashara bilionea Donald Trump kutoka chama cha Republican akimshinda mpinzani wake Hillary Clinton kutoka chama cha Democratic.
Matokeo yalikuwa yakirushwa live katika vituo mbali mbali na vyombo vya habari kama BBC CCN SKY NEWS na Kadharika.
Ili kushinda nafasi hiyo wagombea hao walitakiwa kufikisha kura za wajumbe yani Electoral Votes 270.
ambapo Donald Trump amepata kura 289 huku Hillary Clinton akipata kura 218.
Donald Trump kura za wajumbe 289, 47.6% idadi ya kura 58,844,024
Hillary Clinton kura za wajumbe 218, 47.6%. idadi ya kura 58,879,610
Bi Hillary Clinton amempigia simu Rais Donald Trump kumpongeza kwa ushindi huo. Rais Donald Trump anakuwa rais wa 45 wa Marekani.
Akiongea mjini Newyork Rais Donald amesema amepokea salam za pongezi kutoka kwa Bi Hillary na yeye amempongeza Bi Hillary pamoja na familia yake kwa ushindani mkali aliouonesha.
No comments