Kesi inayo mkabiri Mwanamuziki Chris
Brown imelazimika kutoendelea sababu ikiwa ni ushahidi uliokusanywa na polisi
kutojitosheleza. Kesi hiyo ilitarajiwa kupelekwa kwa waendesha mashtaka wiki
mbili zilizopita ila ilipigwa chini kutokana na ushahidi kutoridhisha.
Kesi hiyo ni kuhusu kitendo cha jinai
ambacho Chris
Brown anatuhumiwa kilikuwa ni kumfukuza Baylee Curran kwa kumnyooshea
bunduki nyumbani kwa Chris ambapo Mwanamuziki (Chris) alikua anafanya sherehe.
Chris alikamatwa mwezi wa nane na
polisi kuchukua maelezo yake na alipaswa kufikishwa mahakamani wiki mbili
zilizopita. Lakini mamlaka zinazohusika zimeshindwa kupata ushahidi wa kutosha
kuweza kumfikisha mahakamani.
No comments