UBUNIFU WA PISHI LA CHAPATI NA MAYAI "ROLEX" LA VUTIA WATALII UGANDA
Pishi la Rolex ambaloni maarufu nchini Uganda ambalo hutengenezwa kwa kukaanga chapati na mayai pekeyake kisha huambatanishwa pamoja na viungo kama vile nyanya, kabichi na vitunguu na kisha kuzungushwa tayari kwa kuliwa limeonekana kuwavutia sana wataliii nchini humo.
Uganda imefanya tamasha la kwanza lengo likiwa ni kuwaonjesha watalii baadhi ya vyakula ambavyo hupendelewa nchini humo.
Awali Rolex kilikua ni chakula cha jioni. CEO WA HOT BONGO 255 alibahatika kushuhudia tangu kuanza kwa pishi hilo ambalo hapo awali watu wengi walipenda kula chakula hicho nyakati za jioni wakikisindikiza na vinywaji kama vile soda, Yoghut na Katunda juice lakini kadri siku zilivyo songa wapishi waligundua uhitaji wawateja wao hivyo kuanza kutengeneza pishi hilo kuanzia asubuhi mpaka jioni.
chini ni baadhi ya picha zilizopigwa na bbc swahili kutoka katika Tamasha la Rolex.
No comments