Mshirikishe mwenzako
Kilimanjaro Queens wa Tanzania wameibuka mabingwa wa Cecafa upande wa kina dada 2016 baada ya kuwashinda Harambee Starlets wa Kenya 2-1 mjini Jinja, Uganda.
Magoli ya Tanzania yamefungwa na Mwahamisi Omar dk 28, 45, Kenya limefungwa na Christina Nafula.
Tanzania walifika fainali baada ya kuwafunga wenyeji Uganda 4-1 mechi ya nusu fainali.
Kenya walifika fainali kwa kuwafunga Ethiopia 3-2.
No comments