Mheshimiwa Joseph Selasini (CHADEMA) ameahidi
atajihudhuru ubunge endapo mradi wa maji wa chigongwe katika manispaa ya Dodoma
utaanza kutoa maji ndani ya siku 21. Alisema hayo juzi katika kamati ya ubunge ya
hesabu ya serikali za mitaa alipofanya ziara katika manispaaa ya Dodoma na
kutembelea baadhi ya miradi ukiwemo wa chigongwe na kubaini kuwa na mapungufu
mengi.
Kauli ya Muheshimiwa Selasini ilikuja
baada ya kaimu mhandisi wa maji Bwana Majuto Eriufoo kuomba kamati hiyo impe
wiki mbili ili maji yaanze kutoka.
No comments