HABARI KUTOKA ABUJA NIGERIA
Wasichana waliotekwa na Boko Haram waelezea jinsi maisha yalivyokuwa baada ya kutekwa.
Wasichana zaidi ya 200 wanafunzi wa shule kutoka Chibok walitekwa na kupelekwa katika ndani zaidi ya Msitu wa Sambisa ambako ndipo kambi ya wapiganaji hao ilipo jiimarisha. Wasichana waliamriwa kuchagua kati ya kuwa watumwa au kujiunga na jeshi la Boko Haram.
Takribani nusu ya wasichana hao walichagua kujiunga na kuolewa na Wapiganaji wa Kundi hilo na wakaondolewa sehemu hiyo nakuto kusikika tena,
Na wale waliokataa walilazimika kuvumilia zaidi ya miaka miwili ya mateso, Kufua kuchota maji, na kuwapikia Boko Haram
Wasichana hao ambao karibia wote walikuwa wakristo, waliishi katika nyumba za nyasi na walilazimishwa kubadili dini kuingia katika uislam. Mwanzoni walikula wali na mahindi.
Na kadri muda ulivyo songa chakula kilipungua na wachache kati yao walikufa kwa njaa.
Baadhi ya watoto hao waliopata chansi ya kuwaona jumapili iliyopita kupitia kituo walicho hifadhiwa kwa ajiri ya matibabu na ushauri walieleza kuwa watoto wao wamekonda sana. wameeleza pia watoto wao wameambia takribani ya wasichana mia moja walikufa kwa kung'atwa na nyoka na mwenzao alifariki wakati wakujifungua.
.
Wasichana hao waliokolewa wiki iliyopita baada ya serikali ya Uswis pamoja na Tume ya kimataifa ya Chama cha Msalaba Mwekundu kufanya mazungumzo na kundi la wapiganaji Boko Harama kuweza kuwaachia wasichana hao
Boko Haram wamekuwa wakifanya matukio kadhaa ya kuuwa wanafunzi lakini tukio la Wasichana 276 waliotekwa kutoka shule ya Chibok Mwaka 2014 Aprili lilitengeneza headline duniani kupeleke maandamano na kampeni ya BRING BACK OUR GIRLS yani rudisheni watoto wetu.
Wasichana waliookolewa wanaandaliwa kwa ajili ya kukutana na Rais wa nchi hiyo Muhammadu Buhari
No comments