
China imeamua kujenga ngazi ndefu katika jabali la milima ya South West Sichuan Province, ambapo watoto walilazimika kushuka chini umbali wa mita 800 kuweza kufika shuleni.
Ngazi hiyo imejengwa kwa vyuma ili kurahisisha safari ya kushuka na kupanda kijijini huko juu ya milima kuwa rahisi.
Awali wakazi wa maeneo hayo ya mlimani walikuwa wakishuka kwa kutumia ngazi za mdahbibu ambazo ziliweza kuhatarisha maisha yao pindi zikioza. kama picha inavyoonyesha hapa chini...

China inazidi kuongoza kwa kuwa na sehemu hatarishi ambazo zinahitaji ujasiri mkubwa kuweza kupambana na changamoto hizo.
chini ni baadhi ya picha za ngazi hiyo ambayo itawawezesha wakazi wa milimani juu kushuka na kufanya manunuzi ya mahitaji yao kwa wiki.





No comments