Mwanamuziki diamond Platinumz ambaye kwa sasa anatamba na kibao kipya cha salome alichomshirikisha Rayvanny, ikiwa ni marudio ya nyimbo ya Maria Salome ilyofanywa na saida karoli ametirika yafuatayo kupitia interview ya Perfect Crispin
Diamond : Nilizungumza na Saida na mimi kama msanii sipendi mtu achukulie kazi yangu kidharau,
Pia nilizungumza na uongozi wake na kunakiasi pia tulitoa ili kiende kwake na kila income ya publishing mama (Saida) atakua anapata 25%. Lengo ni kuonesha kwamba nyimbo za zamani zilikuwepo nzuri na ukizimodify yani ukiziboresha kwa sasa hivi zinaweza kufika mbali kidunia. nilimsikilizisha wizkid alivyokuja ambaye naye ilimchanganya sana na alitamani hata tuifanye nae. hata juzi kati tukiwa na Jk kwake katika chakula cha mchana na familia yake kwake aliifurahia sana na kuirudia karibuni mara tano.
Diamond aliongeza kuwa kuna aina mbili za salome na tofauti ipo kwenye beat kuna yenye vionjo vya asili zaidi na ile ya club.
No comments