Mwanamuziki Saida Karoli aliyetamba kwa ngoma za asili ya kihaya miaka ya mwanzoni mwa 2000 amefurahishwa na kitendo cha mwanamuziki Diamond Platinumz kurudia kuimba nyimbo ya salome ambayo kwa mda wa siku chache sana imepata watazamaji wengi sana kupitia Youtube.
Katika audio mwanamama Saida amesikika akisema amefurahishwa na kitendo hicho ambacho kimejaribu kumrudisha kwenye chart kiasi cha kutafutwa na wahandishi wa habari kwa ajili ya interview.
Nyimbo ya Maria Salome iliimbwa na Saida karoli ambayo ilichanganywa kwa vionjo vya asili ya kihaya pamoja na kiswahili na kuwekwa katika albu yake ya chambua kama karanga. nyimbo hii ilivuma sehemu nyingi za Africa kama Kenya Uganda Rwanda na DR. Congo kiasi cha kumpelekea Saida kuingia katika tuzo za kora mwaka 2006 katika kipengele cha best female Vocalist.
Sikiliza audio.....
No comments