Mkuu wa wilaya Gabriel Mnyele
ameachia wadhifa wake kwa sababu zake binafsi.
Akizungumza na gazeti la Habari Leo,
Mnyele alisema kwamba “ukiteuliwa na mamlaka husika inatoa taarifa na ukiondoka
mamlaka husika inatoa taarifa kwa hiyo mtafuteni msigwa (Mkurugenzi wa
Mawasiliano Ikulu)” mkuu wa mkoa hakupatikanakuelezea kwa undani uamuzi huo,
lakini gazeti la habarileo limethibitiishiwa na viongozi wa halmashauri ya
Wilaya ya Uyui kuwa amejiuzulu wadhifa huo.
Kwa mujibu wa taarifa yao, mnyele
alipita kila idara za Halmashauri ya Wilaya
hiyo kuwaaga akianzia na ofisi yake.
Taarifa za awali zinasema kuachia
kwake ngazi kunatokana na kutingwa na majukumu mengi binafsi aliyonayo.

No comments