Kupitia kipindi cha 360 clouds Tv
Rais wa Manzese Madee ameeleza sakata lililokuwa likivuma mitandaoni nakueleza
kuwa hakupora simu yoyote na kwamba kilakitu kilifanyika mbele ya polisi. Hivyo
madee alihoji kuwa unaweza kupora kitu kwa kumshirikisha polisi.
Madee anadai chanzo cha mkasa huo ni
mchezo mchafu uliochezwa na wenzake alipokwenda Sweden stock home kushuti video yake ambako alikutana na kasumba
za utapeli kiasi cha kumchelewesha tiketi yake ya ndege ya kuelekea Austria.
Na aliporudi nyumbani Tanzania
alibahatika kupata taarifa ya mmoja wa wadau wale kuwepo nchini. Hivyo Madee
akafanya taratibu za kipolisi na kuweza kumchukulia RB na kufanikiwa kumtia
nguvuni. Hivyo mbele ya makubaliano na polisi mama wa kijana huyo alikubali
kumpa madee kiasi cha pesa pamoja na simu yake mpaka deni lake litapomalizika
ili kijana huyo aweze kuwahi ndege ya kurudi nchi aliyokuwa akifanya shughuli
zake.
Hivyo taarifa za kuwa Madee alipora
simu zilikuwa za uzushi na kutaka kumchafua rais huyo na kumsononesha mwanae
alidai made.
Kwa sasa Madee anatamba na ngoma yake
mpya inayokwenda kwa jina la HELA ambayo imeimbwa na maudhui ya kuelimisha
jamii.

No comments