Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema kuwa noti ya Sh 500 itaendelea
kuwepo katika mzunguko, sambamba na sarafu ya Sh 500 hadi itakapotoweka
mikononi mwa wananchi.
![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_ubAVmLYZvBH_FhTLLH0eqMABtSu5lioX30qnxbuNHRDkzvVNeB02SzFnT3nvrbh5AU94xNzLi1MO2zbRcRU9MeQPj-jnjL8Kj12dQE4LpKUCQMTHni49DnXFXfmCWWGnOCfRHUZuEKib4GLGUcSju41IiFI4HzTjZrBFMD=s0-d)
Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki BoT, Marcian Kobello alitoa ufafanuzi
huo kwa wananchi ili kuondoa uvumi ulioenea kuwa noti hiyo, haitatumika
tena kuanzia Desemba 31, mwaka huu.
Alisisitiza kuwa taarifa hizo si za kweli, ni uvumi unaopaswa kupuuzwa na wananchi.
“Ukweli ni kwamba noti ya shilingi 500 itaendelea kuwepo katika
mzunguko sambamba na ile sarafu ya shilingi 500 hadi itakapotoweka
mikononi mwa wananchi,” alisema.
Katika siku za karibuni kumekuwa na taarifa katika mitandao
mbalimbali ya kijamii kwamba noti hiyo ya Sh 500, haitatumika tena
kuanzia Desemba 31, mwaka huu.
Katika siku za karibuni sarafu ya Sh 500 zimekuwa nyingi, tofauti na
zamani, hali inayoashiria kuwa ndio njia ya kuondoa noti hizo mikononi
mwa wananchi.
Pia noti za Sh 500 zimekuwa zikikataliwa mara nyingi na abiria pamoja
na makondakta katika mabasi ya umma, kutokana na mwonekano wake wa
kuchakaa, hali inayosababisha majibizano kati ya abiria na kondakta.
source BONGO5.
No comments