Followers

Theme images by tomograf. Powered by Blogger.

ENTERTAINMENT

GOSSIP

INTERNATIONAL NEWS

LOCAL NEWS

» » » HAKUKUWA NA UGOMVI KATI YA ALIKIBA NA WIZKIDAYO KATIKA CONCERT YA MOMBASA ROCKS - AIDAN CHARLIE ASEMA



Aidan Charlie ambaye ni meneja msaidizi kutoka kwenye Menejimenti ya mwimbaji staa wa bongofleva Alikiba ameongea kuhusu tuhuma mbalimbali zilizotolewa dhidi ya Alikiba kutokana na show ya Mombasa iliyofanyika weekend iliyopita na zifuatazo ni kauli zake.



  • Sio kweli kwamba Alikiba alisema yeye ni msanii mkubwa Afrika Mashariki hivyo Wizkid ndio alitakiwa kupanda stejini kabla yake, alietoa hizo habari kadanganya.



  • Kilichotokea ni kwamba kiujumla Waandaaji hawakuwa wamejipanga vyema, show ilitakiwa kuanza saa nane mchana lakini wakaipeleka mbele mpaka saa tatu usiku.



  • Ishu ilikua wakati Chris Brown alipofika kuliangalia jukwaa na kuzoea mazingira ilibidi seti yote ya Alikiba iliyopangwa jukwaani iondolewe pamoja na watu wa Ali, hiyo ikafanya Alikiba achelewe kufanya rehearsal ambapo alimaliza saa mbili usiku na kurudi hotelini kwenda kujiandaa na show.



  • Tumerudi tu hotelini tunapigiwa simu kuambiwa mnatakiwa kupanda kwenye stage ikabidi Alikiba arudi uwanjani lakini muda ulikua umeyoyoma na Chris Brown alitakiwa kutumbuiza mapema ili awahi Airport.



  • Hakuna kutunishiana misuli kokote kati ya Wizkid na Alikiba, wawili hawa wako vizuri na walikua wanaongea backstage na Wizkid alimwambia Ali haondoki uwanjani mpaka aone show yake
       SOURCE BONGO TUNE
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

About the Author Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

No comments

Leave a Reply

MOVIE

VIDEO

FASHION

Cat-5

MUSIC