ETO'O ARUDISHWA KATIKA KIKOSI CHA TIMU YA ANTALYASPOR
Katika hali isiyotarajiwa na wengi, Klabu ya soka ya Antalyaspor ya Uturuki imemuweka kikosini mshambuliaji wake Samuel Eto'o katika mchezo unafouata dhidi ya Galatasaray.
Mwenyekiti wa Antalyaspor Ali Safak Ozturk amesema kuwa Eto'o ameomba radhi na mwenye moyo mgumu mithili ya jiwe linalokaa majini na haliingii maji ndio tu anapaswa kutokumsahe.
''Tunatumai atajirekebisha na atakuwa na mchango mkubwa katika timu yetu''Ozturk amekiambia kikosi cha timu hiyo.
Hivi karibuni mshambuliaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 35 aliwekwa nje ya kikosi hicho kutokana na kutoa maneno ya kibaguzi kwa uongozi wa klabu hiyo aliyoyaweka katika mtandao wake wa Instagram akisema kuwa ''yamkini baadhi ya watu hawaniheshimu kwa sababu mimi ni mweusi''
Kamailivyo ripotiwa na BBC swahili
No comments