Hizi ndizo nchi 10
zinazo ongoza kwa utajiri Duniani kama zilivyo tangazwa na Press Room VIP, utaratibu wa kupata orodha hii ulifanyika
kwa kuangalia pato la taifa (gross
domestic product), kwa kuangalia thamani
ya bidhaa zote zilizo kamilika ili kupata thamani ya dola kwa mwaka katika Nchi
hiyo watafiti wameweza kuja na majibu haya huku mataifa yanayo zalisha mafuta
yakiongoza
10. Switzerland
Inajumla ya idadi
ya watu milioni 8, pato la taifa kwa kila mswiz ni dola 56,815, Taasisi za
kibank zinalitunza taifa ili nakulifanya kuwa imara. Muhimu kujua kua matajiri
wakubwa duniani na makampuni makubwa wanamiliki/yanamiliki account katika bank
ya Uswiss na hiyo hupelekea taifa hilo kupata mtaji kwa ajili ya uwekezaji
9. United States
Unaweza shangaa USA kushika nafasi hii, ukizingatia
wingi wa idadi ya watu katika nchi hii ambao ni zaidi ya milioni 300. Pato la
taifa kwa kila mwananchi wa Marekani ni dola 57,045. Uchumi wan chi hii
unaongozwa na sekta teknolojia. System ya kidemokrasia ya taifa hili inawalinda wajasiliamali pia hulinda haki za
wavumbuzi mbali mali.
8. Hong Kong
Hong kong ni moja ya nchi zinazoongoza kwa pato la
taifa (GDP) duniani, ni nchi inayosifika kuwa na bandari kubwa, senta ya
kibiashara duniani ikiwa na magorofa mengi na marefu sana. Nchi hii inasifika
kwa tozo la kodi kwakiwango kidogo ikichochewa na biashara huru. Hong kong ina
idadi ya watu milioni 7.1, pato la taifa kwa kila mtu likiwa ni dola 57,676
7. United Arab Emirates
United Arab Emirates ni taifa dogo lenye ukubwa wa mraba 32, 278
miles (dogo kushinda New York), zaidi ya robo tatu ya uchumi wa taifa hili
hutokana na mafuta huku kiwango kinachobaki kinatokana na sekta za huduma/
utalii/mawasiliano. Taifa hili linashikilia nafasi ya pili katika nchi za
kiarabu baada ya Saudi Arabia.
6. Norway
Uchumi wa Norway unaendeshwa na uvuvi, maliasili na viwanda
vya mafuta, pia inashikilia nafasi ya nane kwa usafirishaji wa crude oil. Nafasi
ya tatu kwa usafirishaji wa gas asilia duniani. Pato lake la taifa ni dola
67,619 na idadi ya watu ikiwa milioni 4.97.
5. Kuwait
Kuwait ni taifa dogo ambalo pato lake la taifa (GDP
per capita ) kwa kila mtu ni dola 71,600. Asilimia 10 ya hifadhi za mafuta
duniani hutoka Kuwait ambayo inasaidia kukuza pato la taifa hilo
4. Brunei Darussalam
Brunei Darussalam unaweza ukadhani ndipo jina Dar es
salam ilipozaliwa, ni taifa dogo lenye uchumi wakitajiri ambalo linasapotiwa na
usafirishaji wa mafuta machafu na gas aslia. Jamiii yake imechanganyikana na wajisiliamali
wazawa na wageni ambao husaidi kukuza nchi kiafya na kiuchumi. Pato la taifa ni
dola 80,335 kwa kila mtu.
3. Singapore
Ni nchi ndogo sana. Pato lake la taifa kwa kila mtu ni
dola 84,821 ni mara tano wastani kila mtu duniani. Singaporean upo free, wenye
ubunifu, ushindani na wenye kubadilika. Ni taifa rafiki kibiashara duniani.
2. Luxembourg
Luxembourg ni nchi iliyo fungwa yani isiyo na bahari
magharibi mwa Ulaya inashika nafasi ya pili katika orodha hii. Pato la taifa
likiwa ni dola 94,167 kwa kila mtu mara tisa kwa kila mtu duniani, uimara na
usalama katika soko huchochea ukuaji wa uchumi wa taifa hili Banking ndiyo
sekta kubwa ya uchumi katika taifa hili
1. Qatar
Qatar ndio inashikilia nafasi ya kwanza katka orodha
hii, pato la taifa likiwa dola 146,011 uzalishwaji wa mafuta unasababisha
aslimia 70 ya kodi inayokusanywa na serikali. Kibaya juu ya taifa hili ni ulazimishwaji
wa kazi (forced labour) kutoka mataifa ya Africa na Asia.
No comments