Hussein Janga amehukumiwa miaka mitatu jela na Mahakama ya Wilaya ya ilala kwa kumuibia Mke wake Saida Mwakitete Dhahabu zenye thamani ya Tsh.milioni 5. mshtakiwa alitenda kosa hilo mnamo tarehe 27 october 2014.
sambamba na kfungo hicho, mshtakiwa ametakiwa kulipa milioni 5 kwa mke wake ambayo ni thamani ya dhahabu zilizo ibwa.
Akisoma Hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Said Mkasiwa alisema upande wa Jamuhuri uliweza kuthibitisha pasi shaka shtaka hilo kupitia mashahidi wake watatu.
Kabla ya kutolewa hukumu hiyo wakili wa serikali aliiomba Mhakama kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo. vile vile mshtakiwa alipewa nafasi ya kujitetea juu ya kifungo hicho alidai kuwa ana matatizo ya kiafya na aliiomba mahakama impe kifungo cha nje
No comments