Mwanariadha kutoka Jamaica Usain Bolt
ameshinda mbio za mita 200 katika michuano ya Olympics huko Rio nchini
Brazil na kujinyakulia medali ya dhahabu ya pili baada ya kunyakua ya
michuano ya mbio za mita 100.
Ameshinda mbio hizo za
mita 200 kwa kutumia sekunde 19.78. Bolt kwa sasa anahitaji kushinda
mbio za mita 4x 100 za kupokezana vijiti ili kukamilisha medali ya tatu
ya dhahabu kama alivyofanya katika michuano iliyopita.
Bolt alivunja record ya dunia na kuitwa Mtu anayeongoza kwa speed duniani baada ya kukimbia 200m kwa sekunde 19.30 BEIJING mwaka 2008 na mwaka uliofata kuivunja record hiyo zaidi kwa kukimbia kwa sekunde 19:19 200m huko BERLIN.
Kwa sasa ndoto za mwanariadha huyo zilikua ni kuvunja record alizo weka hapo awali kwa kukimbia sekunde 19 kitu ambacho ameshindwa kutimiza japo amefurahia kujinyakulia medali za dhahabu katika mbio za 100m na 200m
Ifahamike pia Usain Bolt anashikilia record ya dunia kwa kunyakua medali za dhahabu mara tatu mfululizo katika mashindano ya Olympic yani mwaka 2008 BEIJING, 2012 LONDON na 2016 RIO
Ushindi wa Bolt katika 200m
2008 Olympic Games, Beijing | 19.30secs - world record |
2009 World Championships, Berlin | 19.19 - world record |
2011 World Championships, Daegu | 19.40 |
2012 Olympic Games, London | 19.32 |
2013 World Championships, Moscow | 19.66 |
2015 World Championships, Beijing | 19.55 |
2016 Olympic Games, Rio | 19.78 |
No comments