Maji ya Madafu ni kikata kiu kizuri sana na chenye Radha ya kipekee,lakini kinywaji hiki ukiachilia radha yake nzuri na utamu wake kina faida nyingi na zenye manufaa katika mwili wako na hizi ni faida saba za maji ya madafu.
Hayaongezi Uzito.
Mafuta yanayopatikana katika maji ya madafu ni kidogo sana yaani tunaita (Low Fat) na kutokana na uhalisia wake utajisikia kushiba, kwahiyo kwa watu wanaopenda kupunguza uzito ni vizuri ukaacha kunywa soda na ukawa unakunywa maji ya madafu.

Faida katika Ngozi.
Umeshawahi ona watu wanapaka “coconut Butter Lotion”, Vipodozi vingi vilivyo na nazi ni vizuri, kwahiyo unaweza tumia maji ya madafu kutibu ngozi yako, paka mara moja moja maji ya madafu katika ngozi yako, husaidia afya ya ngozi yako.

Dawa nzuri ya Hangover.
Ukiwa umekunywa sana na una hangover pata maji ya madafu asubuhi yakiwa ya baridi, na utaona maajabu, pia inasaidia kukutoa maumivu na ile hali ya kujisikia kutapika. Kwa watumiaji wa kilevi watakuwa wameelewa nachosema.

Mmen’genyo wa chakula.
Maji ya madafu husaidia mmengenyo wako wa chakula , kwahiyo ukipata maji ya madafu baada ya chakula itakusaidia kujisikia vizuri, na kukuweka mbali na matatizo kama kiungulia n.k

Faida kwa Wana Mazoezi.
Unapokuwa unafanya sana mazoezi, au hata katika mizunguko na kazi za kawaida mwili unapoteza maji mengi sana, lakini maji ya madafu yana madini ya potassium ujazo wa miligramu 294 na miligramu 5 za sukari hii kuleta nguvu mwilini na kusaidia mwili usipoteze maji mengi tofauti na vinywaji vingine watu wanavyo vitumia. Kama soda na juice au Maji.

Inapunguza Shinikizo La Damu.
Maji ya Madafu yanaweza kusaidia mzunguko wako wa damu kuwa wa kawaida hii husaidia kukuepusha na shinikizo la damu (Blood Pressure) hasa kama utakuwa unakunywa maji haya mara kwa mara na inashauriwa kunywa maji haya kila siku asubuhi kusaidia kuweka usawa wa eletroliti mwilini.

Ina Viambatanisho muhimu.
Maji ya Madafu yana viambatanisho kadhaa ambavyo vina umuhimu na faida mwilini ambavyo utavipata kiasili tofauti na vivywaji tunavyokunywa vya kiwandani, kwenye maji ya madafu utapata Kalisiamu, Magneziamu, fosiforas, potasiamu. Na sodiamu.

No comments