Kamati ya
mawaziri wa mikopo ya serikali za wanafunzi wa Elimu ya juu nchini
Tanzania inayoundwa na mawaziri, Manaibu waziri na makatibu wa wizara ya
mikopo kutoka vyuo vyote nchini leo July 16 2016 wamkutana na waandishi
wa habari jijini Dar es salaam.
Akizungumza
kwa niaba ya kamati hiyo, Mwenyekiti wa kamati Taifa, Shitindi Venance
amesema kipindi cha mwisho wa mwezi huu wanafunzi wa elimu ya juu
watatakiwa kufika katika vituo vyao vya kazi vilivyosambaa nchi nzima
ili kuendelea kupata mafunzo kwa vitendo ila wamesikitishwa kwamba
wakati wakijiandaa na hilo hakuna mchakato wowote unaoendelea
kupelekea kupata fedha hizo, Shitindi amesema…….
>>>Mpaka
sasa hivi tukiwa tumebakiwa na takribani siku tano kabla ya kufunga
chuo hakuna hata karatasi za kusaini zilizotumwa vyuoni ili kukamilisha
zoezi hilo na mchakato wa kusaini hukuchukua muda wa siku tatu mpaka
tano
>>>Kutokana
na ucheleweshaji huo tunatoa muda wa saa 72 kuanzia leo Jumamosi, mpaka
Jumanne ya wiki ijayo kwa bodi ya mikopo kufikisha fedha za kujikimu
wakati wa mafunzo kwa vitendo katika vyuo vyote hapa nchini ili
wanafunzi waweze kusaini na kupokea malipo yao:-Shitindi
BONYEZA KUTAZAMA
BONYEZA KUTAZAMA
No comments