Msanii wa bongo fleva Shilole,juzi alilalamika kupitia akaunti yake ya instagram kuwa amefanyiwa udhalilishaji kwenye kivuko cha kigamboni lakini hakutaja ni kitu gani hasa amefanyiwa.
Alipoulizwa kuhusu tukio hilo kwenye mahojiano yake na radio 5 Shilole alidai kuwa mmoja wa watumishi wa kivuko hicho alimtaka ashuke kwenye gari lake kama ilivyo utaratibu wa kivuko lakini Shilole alijitetea kuwa alikuwa anaenda kwenye show na isingekuwa sawa yeye ashuke kujichanganya na watu na alipojaribu kumwelewesha mtumishi huyo Shilole amedai kuwa mtumishi huyo alimtolea maneno ambayo siyo ya staha.
“..Unajua msanii hutakiwi kuonekanaonekana kwa sababu thamani yangu mimi ni pale ninapoonekana,mimi nilikuwa naenda kwenye show nikapitia kwenye kivuko cha kigamboni(panton),mfanyakazi akanifuata akataka nishuke kwenye gari lakini mimi nikajaribu kumwelesha jinsi mambo yalivyo lakini majibu aliyonipa hayakuwa mazuri mpaka mtu unajiuliza huyu mtu alipania kwamba akikutana na mimi nitamkoma au” alifunguka Shilole na kuwataka watu wathamini wasanii wa nyumbani.
No comments