Klabu ya Mbeya City ya jijini Mbeya kwa sasa imeweka kambi Matema Beach Kyela Mbeya kwa muda kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu soka Tanzania bara,Mbeya City ambayo inafundishwa na kocha kutoka Malawi Kinnah Phiri, imeweka wazi baadhi ya taarifa zake kuhusu usajili.
Mbeya City kupitia afisa habari wake Dismas Ten imethibitisha kukamilisha usajili waMohamed Mkopi na Rajab Zahir hadi sasa, Kwa upande wa golikipa Juma Kasejaambaye wengi tunafahamu kuwa kamaliza mkataba na Mbeya City, vipi mipango ya klabu imeachana nae jumla au tutaendelea kumuona akiidakia Mbeya City msimu ujao?
“Kuhusiana na usajili hadi sasa Mbeya City imefanikiwa kusajili wachezaji wawili Mkopi na Rajab Zahir, kuhusu mapendekezo gani mwalimu kapendekeza katika usajili hiyo inabakia kuwa siri kwa uongozi, ni kweli Kaseja kamaliza mkataba na Mbeya City na bado mapema siwezi kusema kama tutakuwa nae msimu ujao au la”
No comments