Jina lake kamili
ni John Okafor ila wengi hupenda muita MR. Ibu kutokana na movie iliyompa
umaarufu aliyoigiza na Ukwa.
Kupitia kipindi
cha Saturday Beats muigizaji huyo wa vichekesho ameeleza jinsi alivyo taabika
mwaka 1997 mpaka kufikia hatua ya kutaka kujiua.
HOT BONGO
inakupa full story ya maisha ya msanii huyo kama ifuatavyo.
“unajua
nilipanga kujiua huko AJAO. Siku hiyo nilipanga kujiua kutokana na mazingira
magumu yaliyo nikabili.
Siku tatu kabla
nilikua sijala chakula na nilikua sina matumaini ya kupata chakula wiki moja
mbele. Nilikuwa nikinywa maji tu na sikuwa napenda kubugudhi mtu.
Marafiki zangu
wakaribu hawakujali usalama wangu japo kuwa walijua sikua vizuri kifedha. Nakumbukua
tarehe 18 Desemba 1997 rafiki yangu niliyekuwa nikiishi kwake aliniambia
asubuhi kuwa angesafiri kwao kwa ajiri ya chrismas na hakupenda mtu yeyote
aingie chumbani kwake.
Nikamuhakikishia
kuwa hakuna mtu atakayeingia chumbani kwake, lakini akasema kuwa hata mimi
nitoke . nilimuambia kuwa sina sehemu yoyote ya kuishi na nilimsihi aendelee
kuniamini kama kawaida na ningeendelea kumtunzia chumba chake. Japo nilikuwa
mkubwa kwake, lakini nilifanya kazi zote za kufua kuosha vyomba nilifua mpaka
nguo zake za ndani.
Nilifanya yote
hayo ili niweze kupata pakulala, ila kwa hasira rafiki yangu alitoa vitu vyangu
nje na kuvitupa na kuniambia niondoke kwake. Hivyo alifunga mlango wake na
kuondoka.
Pale nilipokuwa
nimekaa kwa mbele kulikuwa na kisima nilifikiria kuwa sio jambo jema kujirusha
katika kisima na kuyamaliza maisha yangu kwa kujiua na endapo rafiki yangu
angerejea nakukuta nimejiua angejisikia vibaya kwa kuamini kuwa yeye ndiye
chanzo cha mimi kufanya hivyo. Hata watu walio kuwa wakitumia maji yale
wangekuta maiti yangu wasingetumia maji yale.
Lakini nilikwenda
kisimani na kufungua mfuniko wa kisima na pindi nikijiandaa kuruka nilipitiwa
na picha ya mama katika fikra zangu. Nilirudisha mfuniko na kuwaza mama
amejuaje kuwa nataka kujiua.
Mama yangu
alikuwa hai kipindi hicho akiwa na miaka kama 80 hivi. Nilikwenda karibu na
ukuta wa jirani na kuegemea Francis alikuwa akipiga nyimbo ya Michael Bolton “when
am back on my feet again” nikachukua uamuzi wakuto jiua tena.
Baada ya hapo
niliamua kuwa na lala chini ya uvungu wa lorry bovu sehemu ambayo mbwa walikuwa
wakilala nilibaini kuwa ni mbwa walikuwa wakilala pale wakati wa kupasafisha. Ila
sikua na namna zaidi ya kulala pale pale.
Usiku mmoja
takribani mbwa 30 walikuwa wakibweka hivyo hakuna aliye lala nanilizamika
kuhamisha makazi yangu, wakati nikihama nikaona kikundi cha watu wamekusanyika
na nilipo sogea nikagundua kuwa ni maigizo na ndipo hapo nilipo muona Sandra
Ezeh.
Sandra alipo
niona alinikumbatia na kudai kuwa alikuwa shabiki mzuri wa maigizo yangu, hasa
uhalisia wangu katika igizo la Ikuku (muda huu MR IBU aliigiza lakini malipo hayakuweza mnufaisha).
Aliniuliza kuwa kama nilikuwa nafanya chochote na nilopo mwambia kuwa nilikuwa
sina kitu chochote alinisihi tukamuone boyfriend wake.
Nilikubali kwa
vile kwa wakati huo nilikuwa na njaa kali sana. Hivyo tulienda na tulipofika
kwake tukaambiwa amesafiri. Akaniomba twende kwa rafiki yake mwingine.
Tulikutana na
mwanamke mmiliki wa bar niliomba chakula nikapewa nikala na kulala usingizi
mzito sana. Nilipo amka nikaona kibao adetola street nikakumbuka kuna rafiki
aliniomba nikaishi kwake nyumba namba 125. Nilikwenda na nikakuta rafiki yangu
Frank amerejea kutoka London.
Frank alinitaka
nikachukue mizigo yangu ili niishi nae. Nilifata mizigo na kurudi kwake na hapo
ndipo alipo nikabidhi chumba katika ghrofa yake. Nilipiga magoti nakushukuru
Mungu”.
Hii ndiyo story
ya kusikitisha aliyopitia Muigizaji huyo kutoka Nigeria ambaye kwa sasa
anamafanikio makubwa aliyo yapata kutokana na maigizo yake huku akifanya show nyingi ndani na nje ya Afrika. Hivyo hupaswi
kukata tama katika maisha pambana kwa kila namna kuhakikisha unafanikiwa na
unatimiza azma yako.

No comments