Muungano wa wanasheria nchini Gambia
umesema kuwa kitendo cha Rais wa nchi hiyo Yahya Jammeh kukataa matokeo
ya kura zilizoonyesha kuwa ameshindwa katika uchaguzi uliopita ni
kuisaliti nchi hiyo.
Hapo awali Jammeh alikubali kushindwa na kuahidi kuondoka madarakani lakini aliyakataa matokeo hayo siku ya Ijumaa.
Ujumbe wa wakuu wa nchi za Afrika unatarajiwa kusafiri kuelekea Gambia siku ya Jumanne kwa lengo la kuzungumza na Jammeh ili kuachia madaraka.
Marekani imeonya kuwa nchi hiyo inapitia katika mazingira magumu huku baadhi ya viongozi wa kijeshi wakitajwa kumuunga mkono Jammeh.
Ujumbe wa wakuu wa nchi za Afrika unatarajiwa kuwajumuisha Rais wa Nigeria, Ghana, Liberia na Siera Leone.
Kwa upande wake Baraza la usalama la umoja wa mataifa linajadili namna ya kutatua mgogoro huo leo.
SOURCE BBC SWAHILI

No comments